top of page

Jackson Supakila "Mkaliwenu"

Msanii wa maigizo anayefanya vizuri hivi sasa katika upande wa uchekeshaji, anajulikana kwa jina la Mkaliwenu japokuwa jina lake halisi ni Jackson Supakila. Mkaliwenu ni miongoni mwa waigizaji waliochini ya kampuni ya Timamu African Media ambayo imetengeneza filamu nyingi na kupata tuzo za kimataifa nchini Nigeria, Tanzania, USA, Burundi na maeneo mengine. 

Umaarufu mkubwa ambao Mkaliwenu ameupata ni kutokana na mtindo wake mpya wa kuigiza vipande vidogo vidogo na kuvirekodi kisha kusambazwa kwenye mitandao yote ya kijamii, katika kipindi kifupi sana Mkaliwenu amekuwa gumzo mtaani kwa kila mwenye stress na anatamani kupata kitu cha kumchekesha. Vile vile Mkaliwenu amekuwa kipenzi cha watu wengi hasa ambao ni wafuatiliaji wa mitandao ya kijamii.

Ili kupata video zake ambazo anatengeneza kila mara na kuzipost kupitia Youtube channel ya Timamu TV Bonyeza hapa >>

NEW VIDEO

MY PHOTOS

VIEW MY PHOTOS
INTERVIEWS

Please

SUBSCRIBE

kupata video mpya

Sponsors:

  • White Facebook Icon
  • White Twitter Icon
  • White YouTube Icon
  • White Instagram Icon

©2016 by Timamu African Media

bottom of page